A Non-Governmental Organization in Formal Consultative Relations with UNESCO
[English] [French] [German] [Hindi] [Mandarin] [Nepali] [Persian] [Portuguese] [Spanish] [Swahili]
Kwa kuzingatia Kanuni za ICTM na Tamko la Kanuni za Maadili na Uadilifu wa Kitaaluma;
Kwa kuzingatia utume wa ICTM wa kuleta pamoja wasomi wa muziki na densi, wasanii, wanaharakati wa kitamaduni, watunga sera; pia kuwaleta pamoja watu binafsi, shirika mbali mbali, pamoja na taasisi zinazolenga kuhakikisha usawa, ushiriki wa kijamii, haki za binadamu, na uendelevu katika sanaa za maonyesho;
Kufaidika kutokana na muundo mpana wa ushirika wa kimataifa, ujumuishaji wa mila tofauti ya wasomi ulimwenguni, malengo mahususi, pamoja na mada maalum ya vikundi vya utafiti kulingana na jiografia;
Kukubali hitaji la kuheshimu lugha zingine isipokuwa Kiingereza, kukubali maadili yao, pamoja na kutambua nguvu zao za dhana;
Kuzidi kutambua maelekeo ya utafiti, maadili, na jitihada za kisiasa zinazolenga utu na usawa wa binadamu zilizoletwa kwenye ufahamu kutokana na utetezi wa kupambana za ubaguzi wa rangi uliopewa kipao meble upya hivi karibuni na harakati za ‘black lives matter’;
Kutambua hitaji la shirika kama ICTM kuchangia kwenye utafakari na ubunifu wa shughuli za kupambana na ubaguzi au mapendeleo kwa misingi ya utaifa, rangi, kabila, lugha, dini, jinsia, ujinsia, umri, aina ya mwili, ulemavu, historia ya kiuchimi ya jamii, cheo kazini, nadhira na mbinu za utafiti na misingi mingine; na
Kutambua zaidi kuwa mazoea kama haya yamekita mizizi katika taasisi mbali mbali, mitazamo ya kibinafsi; yanadhihirishwa katika uongozi wa kitaaluma, soko la ajira, kwenye mazoea ya uchapishaji, uendeshaji wa mashirika ya ufadhili, na pia katika asili ya kazi yetu inayozidi kuwa hatari;
ICTM inaelezea dhamira yake yakuendeleza shughuli zake kulingana na mitazamo iliyotajwa hapa inayohusika kuondoa ukoloni katika masomo ya muziki na densi pamoja na miundo misingi ya ICTM.
Orodha ya shughuli zilizotajwa hapa chini zinalenga kuhusisha wanachama mbali mbali katika mazungumzo kutoka mitazamo tofauti:
Mfulululizo wa Majadiliano ya ICTM mkondoni yataandaliwa, kila moja ikizingatia mada maalum, na washiriki tofauti wanaohusika katika idara tofauti kama: utafiti, nyaraka, ualimu, ulinzi na uendelevu wa muziki, densi na pamoja sanaa mbali mbali. Katika kila kikao, somo moja au zaidi zinazohusu haki za binadamu, kutoa ukoloni, na mada husika zitawasilishwa kwa mapema kwa wahusika wote pamoja na hadhira. Kamati ya kuratibu iliyoteuliwa na Bodi ya Utendaji itaalika Vikundi vya Utafiti, Kamati za Kitaifa na Kikanda, na wanachama wakijumla kuwasilisha mapedendekezo ya kuandaa na kuongoza vikao hivi.
Kama sehemu ya utafiti wa ICTM 2020, wanachama wataalikwa kutambua, kuelezea, na kupendekeza jinsi ya kupambana na vitendo vya kibaguzi au upendeleo vinavyopatikana katika hafla za ICTM au kuhusiana na uchapishaji wa ICTM, katika mazingira ya kazi mbali na ICTM, na katika sekta tofauti ya kielimu.
Kamati ya Bodi inayohusika na uwepo wa mtandao itazingatia njia za kuboresha matumizi ya vikao vya mtandao vya ICTM ili kujumuisha anuwai ya yaliomo na kuhusisha utofauti mkubwa wa washiriki na hadhira.
Kamati ya Utendaji inayohusika na Maud Karpeles, Young Scholars, na mashikika mengine ya kifedha kama haya, itafuatilia mbinu za kuboresha nafasi za kushiriki katika hafla za ICTM zilizoandaliwa na wanafunzi,wanachama vijana wa taaluma, pamoja na wanachama kutoka mikoa iliyo na uwakilishi mdogo katika ICTM pamoja na/ au mikoa inayo kabiliwa na changamoto za kiuchumi.
Mkutano wa Rais utaandaliwa kuzungumzia mada zilizotajwa hapo awali. Pia, mada hizi zitafuatiliwa na kujumuishwa katika Mkutano wa Dunia wa 2022.
Bodi ya untendajiitaendelea kujadili ubuni wa kifaa cha kuripoti matukio ya kudhulumiwa, kunyanyaswa au tukio vingine vyote katika hafla za ICTM.
Bodi ya utendaji itaendeleza kujadili njia za kuboresha utawala wa kamati za bodi ili kuashiria dhamira ya ICTM kuondoa ukoloni.
Translators: Steve Masai and James Nderitu